Skip to main content
Skip to main content

Maandamano dhidi ya serikali

  • | BBC Swahili
    10,632 views
    Duration: 1:06
    Tazama video inaonyesha waandamanaji wa Iran wakichana bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vipande viwili na kuharibu sanamu ya aliyekuwa kiongozi wa kijeshi, wakati wa maandamano ya kitaifa yanayochochewa na ugumu wa maisha na matatizo ya kiuchumi. Kwa mujibu wa shirika la Human Rights Activists News Agency (HRANA) lenye makao yake Marekani, maandamano yamesambaa katika miji na vijiji 111 kote katika mikoa yote 31 ya Iran. HRANA inasema kuwa angalau waandamanaji 34 na maafisa wanne wa usalama wameuawa, huku takribani waandamanaji 2,200 wakikamatwa. Machafuko hayo yalianza tarehe 28 Desemba, baada ya wafanyabiashara kutoka madukani kuingia mitaani jijini Tehran kupinga kushuka kwa kasi kwa thamani ya sarafu ya Iran, rial, dhidi ya dola ya Marekani. - - #bbcswahili #iran #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw