Tigray: Vita vibaya kushuhudiwa duniani

  • | BBC Swahili
    734 views
    Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeharibu eneo la Tigray nchini Ethiopia vimeshuhudia makumi ya maelfu wakiuawa na kuwaacha watu wake kwa kiasi kikubwa wakipunguziwa misaada na chakula. Baadhi ya makadirio yanasema zaidi ya watu 150,000 wamekufa kutokana na njaa. Umoja wa Mataifa umemshutumu Tigray na vikosi vya serikali kwa kufanya uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya raia na unyanyasaji wa kijinsia. Pande zote mbili zimekanusha kuvuruga misaada. #bbcswahili #tigray #ethiopia