‘Sijalala, sijala kwa sababu sijui kama mpwa wangu yuko huko’- mafuriko Venezuela

  • | BBC Swahili
    848 views
    Makumi ya watu hawajulikani walipo na wengine wengi wamethibitishwa kufariki baada ya mito mitano katikati mwa Venezuela kufurika kutokana na mvua kubwa inayonyesha. Maporomoko mabaya ya ardhi yamesomba nyumba katika jiji la Las Tejerias, kusini mwa mji mkuu Caracas. Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez anasema mvua ya kiwango cha mwezi mmoja ilinyesha katika muda wa saa nane na pampu zinazotumika kuwasha mfumo wa maji ya kunywa ya umma zilisombwa na mafuriko hayo. #bbcswahili #venezuela #mvua