- 167 viewsDuration: 2:07Wanakijiji wa Olongojo, Oyani katika Mpaka wa Transmara na Migori wanalilia serikali kuwanusuru dhidi ya watu wanaodai ni mabwenyenye walio na lengo la kuwafurusha katika makao yao ya jadi kwa njia ya mkato. Wenyeji hao waliojawa na ghadhabu, wengi wakiwa wakongwe wanadai kuhangaishwa na wanaomezea mate ardhi hiyo huku wakidai zaidi ya vijana 15 walikamatwa kiholela kufuatia mzozo wa mara kwa mara kuhusu mashamba yaliyoko katika mpaka huo. Sasa wanaomba maafisa wakuu wa serikali kuzuru eneo hilo ambalo wanadai kuishi tangu miaka ya sitini.