- 285 viewsDuration: 1:55Serikali imeanza zoezi la kusambaza chakula cha msaada katika baadhi ya maeneo ambayo yameathirika zaidi na baa la njaa katika kaunti za Garissa na Wajir. Akizindua mpango wa usambazaji chakula pamoja na malori ya maji safi ya kunywa, afisa mkuu wa mamlaka ya kuthibiti ukame NDMA, Hared Hassan amesema watu zaidi ya laki moja na themanini wanakabiliwa na njaa katika kaunti ya Garissa huku wengine milioni 2.1 katika kaunti kadha wakiwa wameathirika na ukosefu wa chakula.