Wakazi wa Kaunti ya Murang’a pamoja na wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti wanaitaka serikali ya kitaifa kupitia wizara ya fedha kuweka mikakati madhubuti itakayohakikisha fedha zinatolewa kwa kaunti kwa wakati na kwa utaratibu.
Wakizungumza katika hafla ya utoaji wa karo kwa wanafunzi katika wadi ya Kagunduini Eneobunge la Kandara, wakazi wanasema hatua hiyo itachangia pakubwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya mashinani. Wanasema kuchelewa kwa utoaji wa fedha kwa kaunti kumekuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo, hususan sekta ya elimu.