Skip to main content
Skip to main content

Mzozo wa bwawa la Tala

  • | Citizen TV
    695 views
    Duration: 2:39
    Viongozi kutoka Tala wanalalamikia madai kwamba serikali ya Kaunti ya Machakos inajiandaa kuondoa maji katika Bwawa maarufu la Tala ambalo liko kwenye ardhi ya ekari 3 ili kutoa nafasi ya kujenga eneo la kuegesha magari. Viongozi hao walisema kwamba hata kama kutakuwa na ushirikiano wa umma hakuna juhudi zitakazowafanya wakubali na kuruhusu kuondolewa kwa maji hayo. Bwawa hilo lilijengwa na Chifu wa Mukima ambaye alikuwa akienda nyumba moja hadi nyingine akiwashawishi wamiliki jinsi wanavyoweza kutumia maji hayo. Bwawa hilo ni chanzo cha riziki kwa wengi wanaoishi eneo hilo.