- 784 viewsDuration: 3:09Serikali kupitia idara ya mipango maalum imezuru Kaunti ya Tana river kutathmini Hali ya ukame. Waziri wa mipango Maalum Geoffrey Ruku amesema idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo sawia na mifugo katika vijiji kadhaa yameathirika pakubwa. Aidha mabwawa muhimu yamekauka na kusababisha uhaba mkubwa wa Maji kwa binaadamu na mifugo wao. Baadhi ya wakazi wameeleza jinsi serikali ya Kaunti hiyo imewatelekeza na kuwa ni afueni baada ya serikali kuu kutoa msaada wa chakula na Maji. Waziri Ruku amedokeza kuwa kaunti 23 zimeathirika zaidi na ukame.