- 3,062 viewsDuration: 3:06Chama cha Jubilee kimefanya mageuzi ya viongozi wake huku Jeremiah Kioni akihamishwa kuwa mmoja wa manaibu kinara wa chama hicho, nafasi yake ya Katibu Mkuu ikipewa mbunge wa zamani Moitalel Ole Kenta. Kwenye kikao kilichofanyika katika makao makuu ya chama hicho, naibu kinara wa Jubilee Fred Matiangi ametumia fursa hiyo kukosoa utawala wa rais William Ruto haswa katika mwelekeo wa sekta ya elimu nchini.