Skip to main content
Skip to main content

Ubinafsishaji wa Kenya pipeline

  • | Citizen TV
    121 views
    Duration: 2:22
    Katibu katika wizara ya Kawi Alex Wachira amewataka wakenya kuunga mkono juhudi za serikali kubinafsisha mashirika mbali mbali ya serikali akisema ubinafsisaji wa kampuni ya kenya pipeline utawezesha kupatikana kwa fedha za kufadhili usambazaji wa nguvu za umeme mashinani. Akizungumza huko Ganda eneo bunge la Malindi, Wachira ameeleza kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya hisa kama zile za Safaricom zitasaidia kulipa madeni na kufanikisha upatikanaji wa fedha za kuunganisha umeme kwa watu zaidi.Aidha mbunge wa Malindi Amina Mnyazi amesifia mpango huo akisema nguvu za umeme zitabadilisha maisha ya wakaazi na pia visa vya utovu wa usalama kupungua.