Mkurugenzi wa kituo cha kitaifa cha mawasiliano Charles Owino, amewataka watalaamu wa mawasiliano kuzingatia mwongozo uliotolewa wa kutoa taarifa nyakati za mashambulizi ya kigaidi ili kuepuka kuleta wasiwasi miongoni mwa wakazi.
Akizungumza kwenye warsha ya mawasiliano mjini Garissa, Owino amesema wataalamu hao wanafaa kuwa makini kwenye ulimwengu wa sasa wa kidijitali na matumizi wa akiliunde kwa kuthibitisha taarifa zao kupitia kituo hicho.
Aidha alisisitiza umuhimu wa kutoa habari ambazo hazipi umaarufu magaidi wakati wa mashambulizi.