Shindano la warembo wenye ulemavu wa kusikia

  • | BBC Swahili
    249 views
    Mr. & Miss Deaf International ni mashindano ya warembo na watanashati toka pande zote za dunia yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii hapa nchini Tanzania. Mwandishi wa BBC Frank Mavura ametembelea kambi ambayo walimbwende kutoka Tanzania wamepiga kambi ili kutaka kufahamu machache juu ya ushiriki wao na namna ambavyo mashindano haya yatafanyika. Je umeshawahi kujiuliza warembo na watanashati hao wanaweza kufuatisha midundo ya sauti? #bbcswahili #tanzania #sanaa