wanafunzi bora zaidi katika mtihani wa KJSEA katika Shule ya Msingi Nyakwere huko Rongo, Sebastian Onyango, ameamua kurudia gredi ya tisa kutokana na ukosefu wa fedha za kuendeleza masomo yake.
Sebastian alitaka aruhusiwe kurudia darasa la tisa na kujaribu tena mtihani wa KJSEA mwaka huu ili aweze kupata zaidi ya alama 70 zitakazomsaidia kupata udhamini wa kufanikisha ndoto yake.Licha ya walimu kumchangia pesa kidogo kumsaidia kununua mahitaji ya kibinafsi ili ajiunge na sekondari ya juu, alidinda na kusisitiza kurudia gredi ya 9. Haya ni huku umaskini ukizidi kuwahangaisha maelfu ya wanafunzi ambao wameshindw akuendelea na masomo nchini.