Skip to main content
Skip to main content

Mwongozo wa kudhibiti uchochezi mitandaoni watathminiwa

  • | Citizen TV
    157 views
    Duration: 1:59
    Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) imeanza kutekeleza mfumo mpya wa kufuatilia matumizi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii katika kaunti mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa chuki mtandaoni, uchochezi na itikadi kali. Zoezi hilo lililofanyika mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia ambapo tume hiyo ilikutana na viongozi kutoka mashirika mbalimbali . Mashirika ya serikali, asasi za kiraia, na kampuni za teknolojia zinashirikiana kudhibiti mitandao. Mwongozo uliotolewautasaidia kutambua semi hatari na kuwawajibisha kisheria wanaokiuka kanuni zilizowekwa. NCIC imewataka viongozi wa kisiasa, washawishi, na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwajibika.