- 4,402 viewsDuration: 1:00Mshukiwa katika kifo cha mtoto mmoja na majeruhi watatu katika nyumba za serikali mtaani Mukuru amefikishwa mahakamani. Mshukiwa huyo hakusomewa mashtaka alipofikishwa mbele ya mahakama ya makadara. Idara ya upelelezi wa jinai (DCI) iliomba siku 14 za kumzuilia zaidi ili kukamilisha uchunguzi. Dci itatumia muda huo kurekodi taarifa za mashahidi, kukusanya ushahidi na kumfanyia mshukiwa tathmini ya akili. Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 27 anadaiwa kuteketeza nyumba hiyo na kisha kutoroka. Alikamatwa usiku wa kuamkia leo mtaa wa isinya ambako alikuwa amejificha. .