- 1,128 viewsDuration: 6:53Mwaka unapoanza ni kawaida watu hujiwekea malengo ya maendeleo huku wanawake wengi wakichukua fursa hiyo kuanza vyama vya kuwekeza pesa kwa nia ya kusaidiana na kuinuana kifedha. Hata hivyo asilimia kubwa ya vyama hivyo havifiki mbali wala kutimiza malengo kutokana na sababu mbali mbali. Lakini mambo ni tofauti kwa kikundi kimoja kinachojulikana kama komrades ambacho kinajivunia maendeleo chungu nzima huku kikimpa sifa mwanzilishi wake Elizabeth kwa usimamizi bora. Je ndoto ya Elizabeth ilianzia wapi na ni kipi haswa kinachomfanya awe tofauti na viongozi wengine? Hebu tusikilize simulizi yake katika makala yetu ya kwanza ya mwanamke Bomba mwaka huu.