- 474 viewsDuration: 1:27Hafla ya kuwaapisha majaji 15 walioteuliwa katika idara ya mahakama ya rufaa juma lililopita imefanyika leo katika ikulu ya Nairobi. Hafla hiyo imeshuhudiwa na rais William Ruto, jaji mkuu Martha Koome, majaji wa mahakama ya upeop miongoni mwa mafisa wengine wa idara ya mahakama. Majaji hao sasa wanatarajiwa kusaidia katika kurahisisha utoaji wa huduma za mahakama na uamuzi wa kesi za rufaa ambazo mara nyingi huchukua muda kabla ya uamuzi kutolewa.