Muungano wa upinzani unasisitiza kwamba utamenyana na Rais William Ruto kwenye kinyang'anyiro cha urais pamoja, licha ya madai ya juhudi zinazoendelea za kuwatenganisha. Viongozi hao waliozungumza wakati wa kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama cha DP walisisitiza kuwa watashiriki kampeni za pamoja, ila hawakueleza ni lini watamteua mwaniaji wake wa urais. Hayo yakijiri, waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen ameagiza maafisa wa usalama katika eneo la kati ya nchi kuwajibika na kuhakikisha matukio kama yale yaliyoshuhudiwa wakati wa ibada ya Jumapili iliyohudhuriwa na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua huko Othaya Jumapili iliyopita hayatashuhudiwa tena.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive