Joseph Kinyua, amabaye amekuwa mkuu wa utumishi wa umma astaafu

  • | Citizen TV
    1,854 views

    Baada ya miaka ya kuhudumu kama mkuu wa utumishi wa umma, Joseph Kinyua leo amemkabidhi mamlaka hayo Felix Koskei ambaye sasa ndie mkuu wa utumisi wa umma, chini ya serikali ya Rais William Ruto. Joseph Kinyua aliyeshikilia wadhifa huu tangu wakati wa utawala wa Rais mstaafu Marehemu Mwai Kibaki amemkabidhi mamlaka Koskei huku akitoa shukrani kwa muda aliohudumu na kuwatakia heri waliochaguliwa kuwa mawaziri. Akizungumza baada ya kutoa hotuba yake, Rais William Ruto alimtaja Kinyua kuwa mfanyikazi wa umma aliyejitolea, na kuwa akiongoza shughuli ya mpito kwa njia sambamba.