Skip to main content
Skip to main content

Askofu Muheria akosoa CBE, Ogamba akisema mpito umefikia asilimia 98

  • | Citizen TV
    439 views
    Duration: 3:10
    Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri, Anthony Muheria, ameitaka serikali kutathmini upya mfumo wa elimu wa cbe, akionya kuwa viwango vya elimu nchini vinaweza kuathirika pakubwa. Askofu muheria haswa akikosoa jinsi serikali inavyoshughulikia mpito wa wanafunzi kuingia gredi ya 10. Waziri wa elimu Migos Ogamba amesema kuwa mpito wa wanafunzi kuingia gredi ya 10 umefikia asilimia 98 akisisitiza kuwa serikali imeweka mikakati inavyofaa.