- 14,155 viewsDuration: 3:08Marekani imezindua mradi wa miundombinu ya angatua ya kijeshi wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 71, sawa na shilingi bilioni 9.1 za Kenya, katika kambi ya Kijeshi ya Manda Bay. Hatua hii ikiashiria kuimarika kwa operesheni za usalama wa kikanda na mabadiliko ya msimamo wa Washington kuelekea Afrika Mashariki. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka marekani Christopher Landau aliwasili kwa ndege ya kijeshi kati anga tua ya Manda kuzindua ujenzi wa anga tua mpya yenye urefu wa kilomita 3.