Skip to main content
Skip to main content

Mgomo wa matatu uliopangiwa kufanyika leo watibuka

  • | Citizen TV
    7,508 views
    Duration: 1:15
    Shughuli ya kawaida ya usafiri ilishuhudiwa katika miji ya Garissa na Madogo baada ya wahudumu wa matatu kukosa kutekeleza mgomo uliyotangazwa na maafisa wakuu wa sekta hiyo. Kulingana na wahudumu hao, hawakupokea taarifa yeyote kutoka kwa wakilishi wa muungano wao ya kusitisha huduma zao japo wanaunga mkono mgomo huo wa kitaifa. Wamesema wako tayari kufanya mgomo huo wakati wowote wakiitajika kufanya hivyo ili kushinikiza serikali kuchukua hatua kwa wale wanaoangamiza biashara yao kwa kuteketeza moto.