- 402 viewsDuration: 1:52Kizaazaa kilishuhudiwa katika shule ya upili ya Madogo kaunti ya Tana River wakati wafanyikazi wa shule hiyo walipofanya mgomo kulalamikia kucheleweshwa kwa mishahara yao ya miezi minane. Mgomo huo uliathiri masomo kwa muda baada ya wapishi kudinda kutayarishia wanafunzi chakula chao cha mchana hali iliyosababisha tetesi kutoka wanafunzi ambao walitaka swala hilo lishughulikiwe kwa haraka. Wafanyikazi hao wanasema wameshindwa kukithi mahitaji ya familia zao na sasa wanaishi maisha ya omba omba ilhali wanafanyia kazi shule katika hiyo. Mwalimu mkuu wa shule hiyo Abdighani Abdikadir Nuno alikataa kata kata kuzungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake.