- 637 viewsDuration: 3:45Wanafunzi 300 wa shule ya msingi na sekondari msingi kutoka Jamii maskini huko Kajiado Magharibi wamenufaika na ufadhili wa Elimu kutoka kwa wakfu wa Together with Kenya ambayo inajumuisha kulipiwa karo hadi kiwango cha chuo kikuu. Wanafunzi hao watapata elimu ya bure katika kituo cha Elimu cha Entashat ambapo ujenzi wake umekamilika na kuzinduliwa rasmi, Tayari wanafunzi hao wameanza masomo yao katika kituo hicho ambacho pia kina sehemu ya kutoa mafunzo kwa watu wazima.