- 110 viewsDuration: 1:27Wakazi wa Matondoni kisiwani amu wameitaka serikali ya kaunti kuwatengea sehemu maalum ya kumwaga taka ili kupunguza uchafuzi wa fukwe za Bahari Hindi, jambo ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa samaki. Wakiongozwa na mashirika ya kijamii, wakazi hao wamefanya usafi wa fukwe huku wakilalamikia vifo vya punda wao kutokana na kula takataka hatari.