Skip to main content
Skip to main content

Wafanyabiasha wa Embu wakadiria mamilinio ya pesa baada ya mkasa wa moto

  • | Citizen TV
    2,622 views
    Duration: 1:53
    Mali ya Mamilioni ya pesa iliteketea Jumatatu usiku baada ya moto mkubwa kuzuka katika eneo la Shauri, mjini Embu, na kuwaacha takriban wafanyabiashara 300 wakikadiria hasara kubwa. Moto huo, ulioanza majira ya saa tatu usiku, ulienea kwa kasi katika eneo lenye maduka ya kutengeneza na kuuza samani pamoja na maghala ya mbao. Kwa muda mfupi, moto huo uliteketeza bidhaa zilizokamilika, malighafi na mashine za kazi, huku wafanyabiashara wakishuhudia kwa huzuni juhudi zao za miaka mingi zikiungua bila kuweza kuokoa chochote. Polisi wanachunguza kiiini cha mkasa huo wa moto.