Mackenzie Fc ndio mabingwa wa kandanda katika makala ya nne ya Tala Open yaliyokamilika hivi karibuni. Hii ni baada ya kuwashinda shule ya upili ya Upper Hill kutoka Nairobi kwa mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti.
Kwa upande wa akina dada, shule ya upili ya Katani iliibuka mshindi baada ya kuilaza Raila Educational Centre 1–0. Mashindano haya hushirikisha shule kutoka kaunti ya machakos na kaunti jirani za makueni, kitui, nairobi na embu. Kwenye handiboli St. Augustine matuu day waliibuka na ushindi wa 22–15 dhidi ya shule ya Upper Hill, huku Tala wakishinda Misyani 14–4 kwa mashindano ya shule za wasichana.