- 951 viewsDuration: 3:01Hali ya wasiwasi imetenda katika eneo la Rangwe kaunti ya Homa Bay baada ya wenyeji waliojawa na ghadhabu kuteketeza nyumba sita za mwalimu mmoja mkuu. Inadaiwa mwalimu mkuu huyo alimuua mwalimu mmoja mstaafu na mkewe kufuatia mzozo wa ardhi. Maafisa wa polisi kaunti ya Homa Bay kwa ushirikiano na wenzao wa Ujasusi wanaendeleza msako wa mshukiwa ambaye alitoroka baada ya tukio.