Huduma ya Misitu Kenya (KFS) imesisitiza kuwa haitaruhusu ujenzi wowote haramu ndani ya ardhi ya misitu , ikithibitisha kuwa ilizuia usafirishaji wa vifaa vya ujenzi vilivyokusudiwa kujenga upya Shule ya Msingi ya Loramoru, iliyobomolewa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhifadhi wa Misitu wa Kaunti ya Baringo, Ann Nyaoke, alisema shule hiyo iko ndani ya msitu uliolindwa kisheria. Alieleza kuwa, kupitia kwa Mkurugenzi wa Elimu, kipande mbadala cha ardhi nje ya msitu tayari kimepatikana na ujenzi wa shule mpya utaanza mara moja.