- 141 viewsDuration: 1:56Viongozi wa muungano wa wauguzi katika kaunti ya Nyamira wametoa ilani ya mgomo ya siku 14, kulalamikia mazingira duni ya kufanyia kazi, pamoja na kazi za sulubu kutokana na idadi ndogo ya wauguzi na uhamisho wa kila mara unaokiuka sheria na haki za wahudumu hao. Wakiwahutubia wanahabari mjini Nyamira viongozi wa muungano huo wameishtumu serikali ya kaunti hiyo kwa kutowaajiri wauguzi kwa kazi za kudumu zenye pensheni, hali inayowalazimu wauguzi hao kufanya kazi ya sulubu katika mazingira duni.