Maafisa wa muungano wa marubani watakiwa kufika mahakamani

  • | Citizen TV
    2,209 views

    Maafisa wa muungano wa marubani wametakiwa kufika katika mahakama ya leba kesho kuelezea kwanini wamekiuka maagizo ya mahakama na kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu. Haya ni huku marubani wa shirika la ndege la Kenya Airways wamesisitiza kuwa hawarejei kazini hadi pale shirika hilo litakapotekeleza matakwa yao. Aidha wametaka uongozi huo kuacha kutumia kifua kama njia ya kuwashurutisha kusitisha mgomo unaonendelea wakisema wako tayari kufanya mazungumzo.