Waziri wa elimu abadili msimamo kuhusu ufadhili wa elimu ya juu

  • | K24 Video
    42 views

    Wanafunzi wa vyuo vikuu wameitaka wizara ya elimu kutenga fedha zaidi katika kufanikisha masomo yao. Haya yanajiri baada yawaziri wa elimu Ezekiel Machogu kukanusha madai yake ya awali kuwa serikali ina mpango wa kuondoa mgao wa kifedha unaotengewa vyuo vikuu vya umma humu nchini. Waziri Machogu amedai alikuwa amewashauri wasimamizi wa vyuo vikuu watafute njia mbadala za mapato na wasitegemee serikali.