Mgomo wa Marubani | Mahakama yawaagiza kurejea kazini

  • | KBC Video
    50 views

    Marubani wa shirika la ndege la Kenya Airways wanaogoma wameagizwa kurejea kazini kesho asubuhi bila masharti yoyote.Jaji wa mahakama ya kushughulikia mizozo kati ya waajiri na wafanyakazi Anna Mwaure kwenye uamuzi wake pia amewaagiza wasimamizi wa shirika la ndege la Kenya Airways wawaruhusu marubani hao kurejea kazini bila vitisho vyovyote au adhabu kwa kushiriki kwenye mgomo.Uamuzi huo umetolewa baada ya mahakama hiyo kuziagiza pande mbili zinazozozana kutafuta suluhisho litakalotoa mwongozo wa mashauriano ya kumaliza mzozo baina yao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #mgomo #KenyaAirways #News #marubani #mahakama