Itailazimu serikali ya marekani kusubiri hadi kesi kuhusu mkataba wa makubaliano na kenya kuamuliwa, ili kutoa pesa za kufadhili sekta ya Afya.
Hili ni kwa mujibu wa balozi wa marekani nchini Susan Burns ambaye amezungumza huko Nyeri, alipozuru hospitali ya rufaa ya kaunti hio kukagua jinsi fedha za taifa hilo zinavyotumika kuendesha mradi wa PEPFAR. Mpango huo unaolenga kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi. Burns hata hivyo amesisitiza kuwa marekani inaendelea kuzifadhili programu zisizo chini ya mkataba huo, uliotarajiwa kuwekeza kima cha shilingi bilioni 2.5 dola za marekani.