Wezi wa mifugo wavamia kijiji cha Lolmolog na kuiba mbuzi 240

  • | Citizen TV
    1,067 views

    Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Lolmolog, kaunti ya Samburu, baada ya wezi wa mifugo kushambulia kijiji hicho na kutoweka na mbuzi zaidi ya 240. Aidha wavamizi hao walimpiga risasi mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 18 ambaye kwa sasa yuko hali mahututi katika hospitali ya Maralal. Wezi hao waliokuwa wamejihami waliwazuia wakazi kutoka nje walipokuwa wakiiba mifugo hao. Japo polisi eneo hilo wanasema kuwa hawajapokea habari kuhusu kisa hicho, wakazi wanaitaka idara ya usalama kuwatuma maafisa zaidi kushika doria na kuhakikisha kuwa mifugo walioibwa wamerejeshwa