Skip to main content
Skip to main content

Wafanyibiashara walalamika Kisii juu ya kufungiwa biashara zao kwa kutolipa pesa za leseni

  • | Citizen TV
    554 views
    Duration: 1:47
    Chama cha wamiliki wa hoteli na Baa mjini Kisii kimekosoa vikali hatua ya serikali ya kaunti ya Kisii kuanzisha msako na kuwakamata wanaodaiwa kutolipa leseni za mwaka uliopita. Wakizungumza mjini Kisii, wafanyibiashara hao wametaja kuhangaishwa na wasimamizi wa kaunti kuwafungia biashara zao wakisema muda waliopewa wa kulipia leseni hautoshi kwani kuna baadhi ambao walikuwa wamefunga biashara zao mwaka jana kutokana na ukosefu biashara. Sasa wanamtaka gavana wa kaunti ya Kisii Simba Arati kuingilia kati mzozo baina yao na maafisa wa idara ya leseni Kisii kwani hatua ya kuwafungia biashara huenda ikaathiri mapato kwa serikali hiyo ya kaunti.