Wazazi wa mtoto wa miezi 6 watiwa mbaroni huko Leparua kwa ajili ya ukeketaji

  • | Citizen TV
    329 views

    Polisi mjini Isiolo wamewatia mbaroni wazazi waliomfanyia ukeketaji binti yao wa miezi sita katika eneo la Leparua eneo bunge la Isiolo Kaskazini.mtoto huyo aliokolewa jumanne na kupelekwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya kaunti ya Isiolo. Kulingana na madaktari, mtoto huyo alijeruhiwa vibaya sehemu zake za siri lakini anaendelea na matibabu