Mahakama yakubali ombi la DPP la kumuondolea naibu rais Gachagua kesi

  • | Citizen TV
    824 views

    Mahakama imekubali ombi la upande wa mashtaka kuondoa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua na wengine tisa ya shilingi bilinoni saba. Hakimu Victor Wakhumile akikubali ombi hilo aliwaonya washtakiwa katika kesi hiyo kwamba wanaweza kukamatwa na kushtakiwa tena na kosa hilo. Upande wa mashtaka ulidai kwamba ushahidi uliopo katika kesi hiyo hauna msingi wowote wakiongeza kwamba bado uchunguzi unaendelea na iwapo watapata ushahidi wa kutosha basi watuhumiwa watafunguliwa mashataka upya