Wahudumu wa afya wa jamii wa Kajiado wapewa marupurupu

  • | Citizen TV
    160 views

    Kaunti ya Kajiado ikishirikiana na serikali kuu imetenga shilingi milioni 22 katika wizara ya afya ili kusaidia wafanyakazi wanaojitolea kwenye matibabu ya jamii mashinani. Washikadau wa sekta hiyo wamesema kuwa kuna umuhimu wa kuwatia moyo wahudumu wa afya wanaojitolea kufanya kazi katika mazingira magumu ya nyanjani. Naibu gavana wa Kajiado Martine Mosisho amezindua mpango wa kuwapa marupurupu wahudumu hao pamoja na vifaa vya kuwarahisishia kazi wanapohudumia wagonjwa. Mradi huu wa kushughulikia wahudumu wa afya umezinduliwa katika kaunti za Kwale, Migori na Kajiado