- 430 viewsDuration: 2:57Wakulima wengi katika jiji la Kisumu wameanza kilimo cha kisasa, ambapo wanatumia jivu la maganda ya nazi kukuza mimea yao. Kulingana na wanasayansi, jivu hilo lina rotuba ya juu na pia linakinga mimea dhidi ya athari ya uvamizi wa wadudu. Na kama anayoarifu Laura Otieno, serikali ya kaunti ya Kisumu inapania kutoa mafunzo kwa wakulima zaidi walioko jijini humo, ili kuimarisha utoshelevu wa lishe.