KUPPET yataka usalama wa walimu kuangaziwa

  • | Citizen TV
    360 views

    Chama cha walimu wa shule za upili (KUPPET), limeitaka tume ya walimu kuwaongezea marupurupu walimu wanaofanya kazi katika maeneo yenayokabiliwa na changamoto za kiusalama, la sivyo iwaondoe maeneo hayo. Kwenye kongamano la kila mwaka la chama hicho kaunti ya Samburu, viongozi wa KUPPET wamesema kuwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo ya Loongewan, Lolmolog, Losuk, Loibornkare na Pura wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na uvamizi wa kila mara.KUPPET inamtaka Rais William Ruto kuangazia maslahi ya walimu. Aidha walimu wanataka fedha za kutosha kufanikisha mtaala wa CBC