- 13,280 viewsDuration: 3:22Kijiji cha Chepkiep huko Mosop kaunti ya nandi kimesalia kwenye kumbukumbu za tanzia ya ajali ya ndege iliyoua watu sita akiwemo marehemu mbunge Johana Ng'eno. Hata hivyo, ni katika kijiji hiki ambapo taarifa ya ushujaa wa mama na bintiye umegonga vichwa vya habari kwa ujasiri wao baada ya ndege kuanguka. Mwanafunzi muuguzi Jacobeth Jeptoo na mamake walitwaa jukumu zito na kujaribu kuokoa maisha ya yeyote pindi baada ya ajali hiyo.