- 146 viewsDuration: 1:13Wakazi wa eneo la Magumu eneo bunge la Kinangop kaunti ya Nyandarua wanalalamikia mpango wa mstawishaji mmoja wa kujenga maziara ya kibinafsi kwenye ardhi ya ekari 69 karibu na Soko Mpya.. Wakisema utakuwa katika lango kuu la kaunti ya Nyandarua kwenye barabara kuu ya Naivasha-Nairobi..Shughuli za kawaida zilitatizika mchana kutwa katika barabara hiyo wakazi wakiwasha moto kupinga hatua hiyo. Wanataka serikali kusitisha mipango hiyo na badala yake kuanzisha mradi utakaowafaidi wakazi kama vile chuo cha kiufundi. Kulingana na serikali ya kaunti mstawishaji huyo alikuwa amepewa idhini ya kupanda miti katika eneo hilo...