Skip to main content
Skip to main content

Baadhi ya viongozi wa kidini wapinga mswada wa maaradi Lamu

  • | Citizen TV
    457 views
    Duration: 2:15
    Viongozi wa kidini katika Kaunti ya Lamu wanapinga mswada mpya unaolenga kudhibiti mashirika ya kidini, ambao unatarajiwa kufikishwa Bungeni hivi karibuni. Wanasema mswada huo una vipengee vinavyoweza kuidhinisha matumizi mabaya ya fedha za umma. Aidha, wamesisitiza kuwa asilimia kubwa ya viongozi wa kidini na wakazi wa eneo hilo hawana taarifa ya kutosha kuhusu maudhui ya mswada huo. Wakizungumza baada ya kikao cha kuhamasisha umma kuhusu mswada huo, viongozi hao wameelezea kutoridhishwa kwao na zoezi la ukusanyaji maoni, wakisema haukufanyika kama inavyotakiwa Kikatiba.