- 200 viewsDuration: 2:24Kaunti ya Busia inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa damu huku wagonjwa wengi wakilazimika kutafuta usaidia katika maeneo mengine na kugharamika zaidi. Ni hali ambayo imeilazimu serikali ya kaunti ya Busia kuwarai wenyeji mara kwa mara kujitokeza na kutoa msaada wa damu ili kuwasaidia wagonjwa. Mkurugenzi wa idara ya afya katika serkali ya kaunti ya Busia daktari Nina Rabare amesema licha ya juhudi kaunti hiyo imeshindwa kupata damu inayohitajika kuwasaidia wagonjwa. Hata hivyo, muungano wa mashabiki wa Man United eneo la magharibi umeanzisha hamasisho kwa wanachama wake na wenyeji kujitokeza kwa wingi kutoa damu.