- 149 viewsDuration: 1:52Wafugaji nyuki zaidi ya 170 kutoka vijiji 24 katika eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale wamepokea mafunzo ya ufugaji nyuki na kuzalisha asali ya kuuza ili kuwainua kiuchumi Mafunzo hayo yalitolewa na shirika la KidsCare na Klabu ya Rotary ya Mombasa Downtown yanalenga pia kuhakikisha wakazi wanapata fedha za kukidhi mahitaji ya watoto ambao wengi wanatoka familia zisizojiweza. Wakazi wakisema wanazalisha asali kwa wingi na kutaka serikali kuwasaidia kutafuta soko la bidhaa hiyo na kuwarahisishia upataji wa vibali vya ubora wa bidhaa.