Skip to main content
Skip to main content

Mradi wa maji Taita Taveta

  • | Citizen TV
    119 views
    Duration: 1:46
    Ni afueni kwa wakazi 1,500 huko Kiwalwa eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji kitakachosaidia katika shughuli za kilimo na ufugaji. Kisima hicho ambacho kimegharimu shilingi milioni kumi pia kitasambaza maji kwa shule ya upili Kiwalwa pamoja na kituo cha afya ambacho kwa muda mrefu kimekumbwa na uhaba mkubwa wa maji. Wakazi wa eneo hilo wakisema sasa watatumia maji hayo kupanda miti ya matunda na kung'oa miti aina ya 'Mathenge' ambayo imekuwa kero kwao