Skip to main content
Skip to main content

Baadhi ya MCA wamesema hoja ya kumtimua Sajaka iko tayari

  • | Citizen TV
    2,522 views
    Duration: 1:26
    Baadhi ya wawakilishi wa bunge la kaunti ya Nairobi sasa wanasema kila kitu kiko tayari kuwasilisha hoja ya kumbandua ofisini Gavana Johnson Sakaja. Wakiongozwa na naibu kiongozi wa walio wachache katika bunge hilo Waithera Chege, wawakilishi hawa wanasema tayari wamekusanya saini za kutosha kuwasilisha hoja hiyo, wakisema wana mashtaka 22 ambayo wanataka kuyatumia kumbandua ofisini Sakaja. Hatua hii ikijiri saa chache baada ya bunge la kaunti ya Nairobi kuidhinisha mkataba wa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na ile ya Nairobi