Skip to main content
Skip to main content

Washukiwa sita wa KWS wajibu mauaji ya Brian Odhiambo, kesi itaanza Juni

  • | Citizen TV
    570 views
    Duration: 1:23
    Washukiwa sita wa shirika la kws walioshtakiwa kwa madai ya kumteka nyara mvuvi Brian Odhiambo januari mwaka jana, wana kesi ya kujibu. Hakimu mkuu wa mahakama ya nakuru kipkurui kibellion ametoa uamuzi huu akieleza kuwa alitilia maanani ushahidi uliowasilishwa mbele yake. Familia ya Brian ikieleza imani kuwa haki itatendeka. Washukiwa sita francis wachira, Alexander Lorogoi, Isaac Ochieng, Michael Wabukala, Evans Kimaiyo na Abdulrahman Ali Sudi walishtakiwa mwezi mei mwaka jana. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe nane mwezi juni ambapo washukiwa watapata nafasi ya kujitetea.