Skip to main content
Skip to main content

Wabunge waomboleza Ng’eno, wetangula amtaaja kama shujaa wa mijadala

  • | Citizen TV
    276 views
    Duration: 1:21
    Uchunguzi wa maiti ya watu sita waliofariki kwenye ajali ya ndege ya mosop kaunti ya nandi umeonyesha kuwa walifariki kutokana na majeraha na kuvunjika sehemu tofauti za mwili. Mpasuaji mkuu wa maiti serikalini johansen oduor akisema kuwa miili hiyo pia ilikuwa na ishara kubwa ya kuchomeka. Haya yamejiri huku.viongozi na wanasiasa mbalimbali wakiendelea kufika nyumbani kwa marehemu mbunge wa emurua dikirr johana ng’eno, eneo la karen, kutoa pole. akiwaongoza wabunge, spika wa bunge la kitaifa moses wetangula ameomboleza kifo cha marehemu ng'eno akisema kuwa bunge limempoteza kiongozi, ambaye mchango wake bungeni utakumbukwa kwa muda mrefu.